Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Dkt. Khamis Mkanachi, akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya mizinga 100 ya kisasa ya kufugia nyuki iliyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa vikundi sita vya wananchi.
Viongozi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Dkt. Khamis Mkanachi, pamoja na viongozi wa Halmashauri na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, wakikagua moja ya mizinga ya kisasa iliyotolewa kwa vikundi vya ufugaji nyuki.
Makabidhiano ya mizinga 100 ya kisasa ya kufugia nyuki kwa vikundi sita vya wananchi kutoka vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Msitu wa Miyenze yakiendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.
Sehemu ya mizinga 100 ya kisasa ya kufugia nyuki iliyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa vikundi sita vya ufugaji nyuki kutoka vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Msitu wa Miyenze, Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.
Sehemu ya mizinga 100 ya kisasa ya kufugia nyuki iliyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa vikundi sita vya ufugaji nyuki kutoka vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Msitu wa Miyenze, Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Bw. Ntiriyo Ezekiel, akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mizinga 100 ya kisasa ya kufugia nyuki kwa vikundi sita vya wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Dkt. Khamis Mkanachi, akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mizinga 100 ya kisasa ya kufugia nyuki kwa vikundi sita vya wananchi.
Afisa Uhusiano wa Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, akizungumza kwa niaba ya Meneja wa Mgodi huo katika hafla ya makabidhiano ya mizinga 100 ya kisasa ya kufugia nyuki kwa vikundi sita vya wananchi.
Wananchi na wanufaika wa mradi wa ufugaji nyuki kutoka vijiji sita vya Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya mizinga 100 ya kisasa iliyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Dkt. Khamis Mkanachi, akiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi pamoja na washiriki wa hafla ya makabidhiano ya mizinga 100 ya kisasa ya kufugia nyuki iliyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
***
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umekabidhi mizinga 100 ya kisasa ya kufugia nyuki kwa vikundi sita kutoka vijiji sita vinavyopakana na Hifadhi ya Msitu wa Miyenze, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuimarisha utunzaji wa mazingira.
Mizinga hiyo imekabidhiwa kupitia programu ya mgodi ya “Biashara Yako, Biashara Yangu”, inayolenga kuinua kipato cha wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka mgodi kwa kuwawezesha kuanzisha na kuendeleza miradi ya kiuchumi inayozingatia utunzaji wa mazingira.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo kwa niaba ya Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu, Afisa Uhusiano wa Jamii, Zuwena Senkondo, amesema Barrick inaamini kuwa maendeleo ya migodi yake hayawezi kutenganishwa na maendeleo ya jamii zinazoizunguka, ikiwemo jukumu la kulinda mazingira.
Amesema katika mwaka 2026, kupitia Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), mgodi huo umeshirikiana na Halmashauri ya Nyang’hwale kufadhili mradi huo kwa kiasi cha Shilingi milioni 20.
“Fedha hizo zimetumika kununua mizinga 100 ya kisasa, vifaa vya kufugia na kuvunia asali pamoja na pikipiki moja kwa ajili ya kurahisisha ufuatiliaji na usimamizi wa mradi,” amesema Senkondo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Ntiriyo Ezekiel, amesema shughuli za kilimo na ufugaji katika maeneo yanayozunguka Hifadhi ya Msitu wa Miyenze zimekuwa zikichangia uharibifu wa uoto wa asili.
Amesema kutokana na hali hiyo, Halmashauri imebuni mradi wa ufugaji nyuki kama mkakati wa kuimarisha uhifadhi shirikishi wa mazingira na kurejesha uoto wa asili, huku wananchi wakipata fursa ya kujiongezea kipato kupitia uzalishaji wa asali.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Dkt. Khamis Mkanachi, ameushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka mgodi kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Baada ya kukabidhi mizinga hiyo, Dkt. Mkanachi amewataka wananchi walionufaika na mradi huo pamoja na wataalamu watakaohusika na usimamizi wake kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Amesisitiza umuhimu wa mradi huo kuleta manufaa ya kiuchumi kwa wananchi sambamba na kuimarisha juhudi za kulinda Hifadhi ya Msitu wa Miyenze.
Tags
habari














